Four Things You Need to Know
(Kenyan Swahili Translation)
MAMBO MANNE UNAYOSTAHILI KUJUA
1. Kwa sababu umevunja sheria ya Mungu, umetenda dhambi kama watu wengine
- Kila atendaye dhambi amefanya uasi kwa Mungu – soma Waraka wa kwanza wa Yohana 3:4
- Hakuna mwenye haki hata mmoja – soma Warumi 3:10
- Wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu – Soma Warumi 3:23
2. Unastahili kuokolewa kwa dhambi zako
- Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu wapingao ukweli kwa uovu – soma Warumi 1:18
- Watu wanawekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu – soma Waebrania 9:27
- Mshahara wa dhambi ni mauti – soma Warumi 6:23
3. Hauwezi Kujiokoa wewe mwenyewe
- Ni kwa nehema pekee kwa njia ya imani mmeokolewa. Wokovu huu hauji kutoka kwa matendo yetu, ili tujivune hila ni kipawa cha Mungu – soma Waefeso 2:8,9
- Wanadamu hawahesabiwi haki kwa matendo ya sheria – soma Wagalatia 2;16
- Yesu alisema, “Mimi ndimi njia, ukweli, na uzima, mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi” – soma Injili ya Yohana 14:6
4. Ni Yesu Kristo pekee anaye weza kukuokoa kutoka kwa adhabu ya dhambi
- Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki ili atulete kwa Mungu – soma Waraka wa Kwanza wa Petro 3:18
- Kwa maana jinsi hii, Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele – soma Injili ya Yohana 3:16
- Karama (Kipawa) cha Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu – soma Warumi 6:23
- Kila amwaminiye Mwana ana uzima wa milele, asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia – soma Injili ya Yohana 3:36
MAMBO MANNE NI LAZIMA UFANYE
1. Ukiri na kuungama dhambi zako kwa Mungu
Soma Waraka wa Kwanza wa Yohana – 1:9
2. Acha dhambi zako
Soma Matendo ya Mitume 17:30
3. Mwamini Kristo Yesu
Soma Matendo ya Mitume 16:31
4. Mwishie Mungu
Soma Wakorintho wa Kwanza 10:31